Pasha®

Mtaalam wa mikate akiwa upande wako

Hamira kavu ya papo hapo

Pasha® ni mojawapo ya chapa ya hamira kavu ya papo hapo iliyo mashuhuri na isambazwayo kwa upana ulimwenguni kote. Chapa hii imekuwa ikitumiwa kwa miongo kadhaa na waokaji, ambao wanatafuta uaminifu na ufanyajikazi bora. Kutumia hamira ya Pasha® inamaanisha kutumia mojawapo ya hamira zilizobora zaidi ziuzwazo na kufanya kazi na “mwokaji mtaalam“.

Jina lake la chapa linahusu waheshimiwa wa ngazi ya juu wa Kituruki chini ya Milki ya Ottoman, ambao walikuwa sehemu ya wasomi wa jamii ya Kituruki. Hivi ndivyo jina Pasha lilivyopewa chachu yetu, kwa kuzingatia ubora wake wa hali ya juu sana, ambao unaifanya kuwa muhimu katika soko la mikate.

Imefungwa chini ya ombwe la hewa, ili kuhifadhi sifa zake zote kwa kipindi cha miezi 24.