KUHUSU SISI...
Istabul DOSU Maya ni mmojawapo wa washiriki muhimu katika tasnia ya uokaji, iliyobobea kwenye kuzalisha hamira ya kuokea na viambato vya kuoka vyenye ubora wa juu kabisa, vilivyobadilishwa ili vifae aina tofauti za utengenezaji mikate ulimwenguni.
Istabul DOSU Maya ni kampuni, iliyoanzishwa Istabul, Uturuki, ambayo kwa msaada wa utaalamu wake, ufundi na ujuzi, imepanda kuwa katika kundi la makampuni tajika kwenye fani ya utengenezaji wa mikate.
Uanuwai na ubora wa anuwai za bidhaa zetu za mikate unafanya tuweze kukidhi mategemeo ya waokaji na walaji ulimwenguni kote.
Ubora, ukawaida na umahiri wa kiufundi ni mali ambazo tunaziweka katika kuwahudumia wateja wetu ili kufanikiwa katika bidhaa za mkate wa kiwango cha juu.